Swahili
Surah Al-Hijr ( The Rocky Tract ) - Aya count 99
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُّبِينٍ
( 1 ) Alif Lam Ra. (A. L. R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha.
رُّبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ
( 2 ) HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.
ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
( 3 ) Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua.
وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ
( 4 ) Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu.
مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ
( 5 ) Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ
( 6 ) Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
( 7 ) Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
مَا نُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذًا مُّنظَرِينَ
( 8 ) Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
( 9 ) Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الْأَوَّلِينَ
( 10 ) Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
( 11 ) Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli.
كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ
( 12 ) Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu.
لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ
( 13 ) Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale.
وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيهِ يَعْرُجُونَ
( 14 ) Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda,
لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ
( 15 ) Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ
( 16 ) Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia.
وَحَفِظْنَاهَا مِن كُلِّ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ
( 17 ) Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye.
إِلَّا مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ مُّبِينٌ
( 18 ) Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kinacho onekana.
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْزُونٍ
( 19 ) Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake.
وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ
( 20 ) Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ
( 21 ) Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu.
وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ
( 22 ) Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka.
وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ
( 23 ) Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi.
وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ
( 24 ) Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari.
وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
( 25 ) Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi.
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
( 26 ) Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ
( 27 ) Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
( 28 ) Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ
( 29 ) Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia.
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
( 30 ) Basi Malaika wote pamoja walimsujudia,
إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ أَن يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
( 31 ) Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu.
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
( 32 ) (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu?
قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
( 33 ) Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ
( 34 ) (Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni!
وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ
( 35 ) Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
( 36 ) Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa.
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ
( 37 ) (Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ
( 38 ) Mpaka siku ya wakati maalumu.
قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
( 39 ) Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ
( 40 ) Ila waja wako walio safika.
قَالَ هَٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ
( 41 ) Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka.
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ
( 42 ) Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ
( 43 ) Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote.
لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ
( 44 ) Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
( 45 ) Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
( 46 ) (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani.
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ
( 47 ) Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana.
لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ
( 48 ) Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.
نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
( 49 ) Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ
( 50 ) Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu!
وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ
( 51 ) Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim.
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ
( 52 ) Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni.
قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ
( 53 ) Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi.
قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
( 54 ) Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ
( 55 ) Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa.
قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ
( 56 ) Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea?
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
( 57 ) Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe?
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
( 58 ) Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu!
إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ
( 59 ) Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا ۙ إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ
( 60 ) Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma.
فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ
( 61 ) Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i,
قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
( 62 ) Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ
( 63 ) Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka.
وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ
( 64 ) Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli.
فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ
( 65 ) Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa.
وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ
( 66 ) Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali.
وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ
( 67 ) Na wakaja watu wa mji ule nao furahani.
قَالَ إِنَّ هَٰؤُلَاءِ ضَيْفِي فَلَا تَفْضَحُونِ
( 68 ) Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe.
وَاتَّقُوا اللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ
( 69 ) Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ
( 70 ) Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
قَالَ هَٰؤُلَاءِ بَنَاتِي إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ
( 71 ) Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji.
لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ
( 72 ) Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ
( 73 ) Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa.
فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ
( 74 ) Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ
( 75 ) Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi.
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقِيمٍ
( 76 ) Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ
( 77 ) Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
وَإِن كَانَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ
( 78 ) Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu.
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ
( 79 ) Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi.
وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الْحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ
( 80 ) Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume.
وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ
( 81 ) Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza.
وَكَانُوا يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا آمِنِينَ
( 82 ) Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ
( 83 ) Basi ukelele ukawatwaa asubuhi.
فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ
( 84 ) Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ ۖ فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ
( 85 ) Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ
( 86 ) Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi.
وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِّنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ
( 87 ) Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu.
لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ
( 88 ) Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.
وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ
( 89 ) Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha.
كَمَا أَنزَلْنَا عَلَى الْمُقْتَسِمِينَ
( 90 ) Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa,
الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ
( 91 ) Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande.
فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
( 92 ) Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote,
عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
( 93 ) Kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
( 94 ) Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina.
إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ
( 95 ) Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli.
الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
( 96 ) Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua!
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
( 97 ) Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo.
فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ
( 98 ) Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.
وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ
( 99 ) Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.