Swahili
Surah At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya count 29
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ
( 1 ) Jua litakapo kunjwa,
وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ
( 2 ) Na nyota zikazimwa,
وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ
( 3 ) Na milima ikaondolewa,
وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ
( 4 ) Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ
( 5 ) Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,
وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ
( 6 ) Na bahari zikawaka moto,
وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ
( 7 ) Na nafsi zikaunganishwa,
وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ
( 8 ) Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ
( 9 ) Kwa kosa gani aliuliwa?
وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ
( 10 ) Na madaftari yatakapo enezwa,
وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ
( 11 ) Na mbingu itapo tanduliwa,
وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ
( 12 ) Na Jahannamu itapo chochewa,
وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ
( 13 ) Na Pepo ikasogezwa,
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ
( 14 ) Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ
( 15 ) Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
الْجَوَارِ الْكُنَّسِ
( 16 ) Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ
( 17 ) Na kwa usiku unapo pungua,
وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ
( 18 ) Na kwa asubuhi inapo pambazuka,
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ
( 19 ) Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ
( 20 ) Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ
( 21 ) Anaye t'iiwa, tena muaminifu.
وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ
( 22 ) Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.
وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ
( 23 ) Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ
( 24 ) Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ
( 25 ) Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.
فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ
( 26 ) Basi mnakwenda wapi?
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ
( 27 ) Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ
( 28 ) Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
( 29 ) Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.