Swahili
Surah Al-Mursalat ( Those sent forth ) - Aya count 50
وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا
( 1 ) Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا
( 2 ) Na zinazo vuma kwa kasi!
وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا
( 3 ) Na zikaeneza maeneo yote!
فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا
( 4 ) Na zinazo farikisha zikatawanya!
فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا
( 5 ) Na zinazo peleka mawaidha!
عُذْرًا أَوْ نُذْرًا
( 6 ) Kwa kuudhuru au kuonya,
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ
( 7 ) Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ
( 8 ) Wakati nyota zitakapo futwa,
وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ
( 9 ) Na mbingu zitakapo pasuliwa,
وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ
( 10 ) Na milima itakapo peperushwa,
وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ
( 11 ) Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ
( 12 ) Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
لِيَوْمِ الْفَصْلِ
( 13 ) Kwa siku ya kupambanua!
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ
( 14 ) Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 15 ) Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ
( 16 ) Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ
( 17 ) Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ
( 18 ) Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 19 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ
( 20 ) Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ
( 21 ) Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ
( 22 ) Mpaka muda maalumu?
فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ
( 23 ) Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 24 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا
( 25 ) Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا
( 26 ) Walio hai na maiti?
وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا
( 27 ) Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 28 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ
( 29 ) Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ
( 30 ) Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ
( 31 ) Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ
( 32 ) Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ
( 33 ) Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 34 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
هَٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ
( 35 ) Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ
( 36 ) Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 37 ) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ
( 38 ) Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ
( 39 ) Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 40 ) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ
( 41 ) Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ
( 42 ) Na matunda wanayo yapenda,
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
( 43 ) Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
( 44 ) Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 45 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ
( 46 ) Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 47 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ
( 48 ) Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
( 49 ) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ
( 50 ) Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?