Swahili
Surah Al-Qiyamah ( The Resurrection ) - Aya count 40
لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ
( 1 ) Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ
( 2 ) Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ
( 3 ) Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ
( 4 ) Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ
( 5 ) Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ
( 6 ) Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ
( 7 ) Basi jicho litapo dawaa,
وَخَسَفَ الْقَمَرُ
( 8 ) Na mwezi utapo patwa,
وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ
( 9 ) Na likakusanywa jua na mwezi,
يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ
( 10 ) Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
كَلَّا لَا وَزَرَ
( 11 ) La! Hapana pa kukimbilia!
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ
( 12 ) Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
( 13 ) Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ
( 14 ) Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ
( 15 ) Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ
( 16 ) Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ
( 17 ) Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ
( 18 ) Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ
( 19 ) Kisha ni juu yetu kuubainisha.
كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ
( 20 ) Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ
( 21 ) Na mnaacha maisha ya Akhera.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ
( 22 ) Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
( 23 ) Zinamwangallia Mola wao Mlezi.
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ
( 24 ) Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ
( 25 ) Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ
( 26 ) La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ
( 27 ) Na pakasemwa: Nani wa kumganga?
وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ
( 28 ) Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ
( 29 ) Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ
( 30 ) Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ
( 31 ) Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.
وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
( 32 ) Bali alikanusha, na akageuka.
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ
( 33 ) Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ
( 34 ) Ole wako, ole wako!
ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ
( 35 ) Kisha Ole wako, ole wako!
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى
( 36 ) Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ
( 37 ) Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ
( 38 ) Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ
( 39 ) Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ
( 40 ) Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?