Swahili
Surah An-Nazi'at ( Those who Pull Out ) - Aya count 46
وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا
( 1 ) Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu,
وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا
( 2 ) Na kwa wanao toa kwa upole,
وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا
( 3 ) Na wanao ogelea,
فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا
( 4 ) Wakishindana mbio,
فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا
( 5 ) Wakidabiri mambo.
يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ
( 6 ) Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ
( 7 ) Kifuate cha kufuatia.
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ
( 8 ) Siku hiyo nyoyo zitapiga piga,
أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ
( 9 ) Macho yatainama chini.
يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ
( 10 ) Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً
( 11 ) Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ
( 12 ) Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ
( 13 ) Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ
( 14 ) Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ
( 15 ) Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى
( 16 ) Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia:
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ
( 17 ) Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ
( 18 ) Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ
( 19 ) Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ
( 20 ) Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
( 21 ) Lakini aliikadhibisha na akaasi.
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ
( 22 ) Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
( 23 ) Akakusanya watu akanadi.
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ
( 24 ) Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ
( 25 ) Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ
( 26 ) Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.
أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ ۚ بَنَاهَا
( 27 ) Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا
( 28 ) Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا
( 29 ) Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا
( 30 ) Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا
( 31 ) Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا
( 32 ) Na milima akaisimamisha,
مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ
( 33 ) Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ
( 34 ) Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ
( 35 ) Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
( 36 ) Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
( 37 ) Basi ama yule aliye zidi ujeuri,
وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
( 38 ) Na akakhiari maisha ya dunia,
فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ
( 39 ) Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ
( 40 ) Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ
( 41 ) Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا
( 42 ) Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا
( 43 ) Una nini wewe hata uitaje?
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا
( 44 ) Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا
( 45 ) Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا
( 46 ) Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.