Swahili
Surah Al-Ghashiya ( The Overwhelming ) - Aya count 26
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
( 1 ) Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ
( 2 ) Siku hiyo nyuso zitainama,
عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ
( 3 ) Zikifanya kazi, nazo taabani.
تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً
( 4 ) Ziingie katika Moto unao waka -
تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ
( 5 ) Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ
( 6 ) Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ
( 7 ) Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ
( 8 ) Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ
( 9 ) Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ
( 10 ) Katika Bustani ya juu.
لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً
( 11 ) Hawatasikia humo upuuzi.
فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ
( 12 ) Humo imo chemchem inayo miminika.
فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ
( 13 ) Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ
( 14 ) Na bilauri zilizo pangwa,
وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ
( 15 ) Na matakia safu safu,
وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ
( 16 ) Na mazulia yaliyo tandikwa.
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ
( 17 ) Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ
( 18 ) Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ
( 19 ) Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ
( 20 ) Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ
( 21 ) Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ
( 22 ) Wewe si mwenye kuwatawalia.
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ
( 23 ) Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ
( 24 ) Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ
( 25 ) Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم
( 26 ) Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!