Swahili
Surah Al-'alaq ( The Clot ) - Aya count 19
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ
( 1 ) Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ
( 2 ) Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ
( 3 ) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ
( 4 ) Ambaye amefundisha kwa kalamu.
عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ
( 5 ) Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ
( 6 ) Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ
( 7 ) Akijiona katajirika.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ
( 8 ) Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ
( 9 ) Umemwona yule anaye mkataza
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ
( 10 ) Mja anapo sali?
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ
( 11 ) Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ
( 12 ) Au anaamrisha uchamngu?
أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
( 13 ) Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّهَ يَرَىٰ
( 14 ) Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ
( 15 ) Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ
( 16 ) Shungi la uwongo, lenye makosa!
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ
( 17 ) Basi na awaite wenzake!
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ
( 18 ) Nasi tutawaita Mazabania!
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩
( 19 ) Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!