Swahili
Surah Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya count 25
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ
( 1 ) Itapo chanika mbingu,
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
( 2 ) Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ
( 3 ) Na ardhi itakapo tanuliwa,
وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ
( 4 ) Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
( 5 ) Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ
( 6 ) Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ
( 7 ) Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا
( 8 ) Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا
( 9 ) Na arudi kwa ahali zake na furaha.
وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ
( 10 ) Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا
( 11 ) Basi huyo ataomba kuteketea.
وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا
( 12 ) Na ataingia Motoni.
إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا
( 13 ) Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ
( 14 ) Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا
( 15 ) Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ
( 16 ) Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ
( 17 ) Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ
( 18 ) Na kwa mwezi unapo pevuka,
لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ
( 19 ) Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
( 20 ) Basi wana nini hawaamini?
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩
( 21 ) Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ
( 22 ) Bali walio kufuru wanakanusha tu.
وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ
( 23 ) Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
( 24 ) Basi wabashirie adhabu chungu!
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ
( 25 ) Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.