Swahili
Surah Al-Waqi'ah ( The Event ) - Aya count 96
إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ
( 1 ) Litakapo tukia hilo Tukio
لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ
( 2 ) Hapana cha kukanusha kutukia kwake.
خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ
( 3 ) Literemshalo linyanyualo,
إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا
( 4 ) Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso,
وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا
( 5 ) Na milima itapo sagwasagwa,
فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا
( 6 ) Iwe mavumbi yanayo peperushwa,
وَكُنتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً
( 7 ) Na nyinyi mtakuwa namna tatu:-
فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ
( 8 ) Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ
( 9 ) Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ
( 10 ) Na wa mbele watakuwa mbele.
أُولَٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ
( 11 ) Hao ndio watakao karibishwa
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ
( 12 ) Katika Bustani zenye neema.
ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ
( 13 ) Fungu kubwa katika wa mwanzo,
وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ
( 14 ) Na wachache katika wa mwisho.
عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ
( 15 ) Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.
مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ
( 16 ) Wakiviegemea wakielekeana.
يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ
( 17 ) Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,
بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ
( 18 ) Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ
( 19 ) Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.
وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
( 20 ) Na matunda wayapendayo,
وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ
( 21 ) Na nyama za ndege kama wanavyo tamani.
وَحُورٌ عِينٌ
( 22 ) Na Mahurulaini,
كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ
( 23 ) Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.
جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
( 24 ) Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا
( 25 ) Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,
إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا
( 26 ) Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama.
وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ
( 27 ) Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?
فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ
( 28 ) Katika mikunazi isiyo na miba,
وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ
( 29 ) Na migomba iliyo pangiliwa,
وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ
( 30 ) Na kivuli kilicho tanda,
وَمَاءٍ مَّسْكُوبٍ
( 31 ) Na maji yanayo miminika,
وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ
( 32 ) Na matunda mengi,
لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ
( 33 ) Hayatindikii wala hayakatazwi,
وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ
( 34 ) Na matandiko yaliyo nyanyuliwa.
إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً
( 35 ) Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,
فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا
( 36 ) Na tutawafanya vijana,
عُرُبًا أَتْرَابًا
( 37 ) Wanapendana na waume zao, hirimu moja.
لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ
( 38 ) Kwa ajili ya watu wa kuliani.
ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ
( 39 ) Fungu kubwa katika wa mwanzo,
وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ
( 40 ) Na fungu kubwa katika wa mwisho.
وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ
( 41 ) Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ
( 42 ) Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,
وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ
( 43 ) Na kivuli cha moshi mweusi,
لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ
( 44 ) Si cha kuburudisha wala kustarehesha.
إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ
( 45 ) Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.
وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنثِ الْعَظِيمِ
( 46 ) Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa,
وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
( 47 ) Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ
( 48 ) Au baba zetu wa zamani?
قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ
( 49 ) Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho
لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ
( 50 ) Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.
ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ
( 51 ) Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,
لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ
( 52 ) Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ
( 53 ) Na kwa mti huo mtajaza matumbo.
فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ
( 54 ) Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.
فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ
( 55 ) Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu.
هَٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ
( 56 ) Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.
نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ
( 57 ) Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
أَفَرَأَيْتُم مَّا تُمْنُونَ
( 58 ) Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?
أَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ
( 59 ) Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
( 60 ) Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ
( 61 ) Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ
( 62 ) Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ
( 63 ) Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?
أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ
( 64 ) Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?
لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ
( 65 ) Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu,
إِنَّا لَمُغْرَمُونَ
( 66 ) Mkisema: Hakika sisi tumegharimika;
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
( 67 ) Bali sisi tumenyimwa.
أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ
( 68 ) Je! Mnayaona maji mnayo yanywa?
أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ
( 69 ) Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ
( 70 ) Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ
( 71 ) Je! Mnauona moto mnao uwasha?
أَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِئُونَ
( 72 ) Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِّلْمُقْوِينَ
( 73 ) Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ
( 74 ) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ
( 75 ) Basi naapa kwa maanguko ya nyota,
وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ
( 76 ) Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!
إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ
( 77 ) Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,
فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ
( 78 ) Katika Kitabu kilicho hifadhiwa.
لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ
( 79 ) Hapana akigusaye ila walio takaswa.
تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ
( 80 ) Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
أَفَبِهَٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ
( 81 ) Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ
( 82 ) Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ
( 83 ) Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ
( 84 ) Na nyinyi wakati huo mnatazama!
وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ
( 85 ) Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ
( 86 ) Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
( 87 ) Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
فَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ
( 88 ) Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,
فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ
( 89 ) Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
وَأَمَّا إِن كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ
( 90 ) Na akiwa katika watu wa upande wa kulia,
فَسَلَامٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ
( 91 ) Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.
وَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ
( 92 ) Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ
( 93 ) Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,
وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ
( 94 ) Na kutiwa Motoni.
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ
( 95 ) Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ
( 96 ) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa.