Swahili
Surah Al-Qamar ( The Moon ) - Aya count 55
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ
( 1 ) Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ
( 2 ) Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
وَكَذَّبُوا وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَكُلُّ أَمْرٍ مُّسْتَقِرٌّ
( 3 ) Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.
وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّنَ الْأَنبَاءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ
( 4 ) Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
حِكْمَةٌ بَالِغَةٌ ۖ فَمَا تُغْنِ النُّذُرُ
( 5 ) Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ ۘ يَوْمَ يَدْعُ الدَّاعِ إِلَىٰ شَيْءٍ نُّكُرٍ
( 6 ) Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha;
خُشَّعًا أَبْصَارُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُّنتَشِرٌ
( 7 ) Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika,
مُّهْطِعِينَ إِلَى الدَّاعِ ۖ يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ
( 8 ) Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ
( 9 ) Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ
( 10 ) Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!
فَفَتَحْنَا أَبْوَابَ السَّمَاءِ بِمَاءٍ مُّنْهَمِرٍ
( 11 ) Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.
وَفَجَّرْنَا الْأَرْضَ عُيُونًا فَالْتَقَى الْمَاءُ عَلَىٰ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ
( 12 ) Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.
وَحَمَلْنَاهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ
( 13 ) Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا جَزَاءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ
( 14 ) Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.
وَلَقَد تَّرَكْنَاهَا آيَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
( 15 ) Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
( 16 ) Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
( 17 ) Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?
كَذَّبَتْ عَادٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
( 18 ) Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي يَوْمِ نَحْسٍ مُّسْتَمِرٍّ
( 19 ) Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,
تَنزِعُ النَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ مُّنقَعِرٍ
( 20 ) Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa.
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
( 21 ) Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
( 22 ) Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka?
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ
( 23 ) Thamudi waliwakanusha Waonyaji.
فَقَالُوا أَبَشَرًا مِّنَّا وَاحِدًا نَّتَّبِعُهُ إِنَّا إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ
( 24 ) Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
أَأُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِن بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ
( 25 ) Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!
سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ الْكَذَّابُ الْأَشِرُ
( 26 ) Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
إِنَّا مُرْسِلُو النَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَارْتَقِبْهُمْ وَاصْطَبِرْ
( 27 ) Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili.
وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ الْمَاءَ قِسْمَةٌ بَيْنَهُمْ ۖ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ
( 28 ) Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika.
فَنَادَوْا صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ
( 29 ) Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
( 30 ) Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَاحِدَةً فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ
( 31 ) Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa.
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
( 32 ) Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ بِالنُّذُرِ
( 33 ) Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبًا إِلَّا آلَ لُوطٍ ۖ نَّجَّيْنَاهُم بِسَحَرٍ
( 34 ) Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
نِّعْمَةً مِّنْ عِندِنَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي مَن شَكَرَ
( 35 ) Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.
وَلَقَدْ أَنذَرَهُم بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا بِالنُّذُرِ
( 36 ) Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.
وَلَقَدْ رَاوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِ فَطَمَسْنَا أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ
( 37 ) Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
وَلَقَدْ صَبَّحَهُم بُكْرَةً عَذَابٌ مُّسْتَقِرٌّ
( 38 ) Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ
( 39 ) Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
( 40 ) Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?
وَلَقَدْ جَاءَ آلَ فِرْعَوْنَ النُّذُرُ
( 41 ) Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَاهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُّقْتَدِرٍ
( 42 ) Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.
أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُولَٰئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَاءَةٌ فِي الزُّبُرِ
( 43 ) Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُّنتَصِرٌ
( 44 ) Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ
( 45 ) Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
بَلِ السَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَالسَّاعَةُ أَدْهَىٰ وَأَمَرُّ
( 46 ) Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ
( 47 ) Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ
( 48 ) Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ
( 49 ) Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
وَمَا أَمْرُنَا إِلَّا وَاحِدَةٌ كَلَمْحٍ بِالْبَصَرِ
( 50 ) Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
( 51 ) Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?
وَكُلُّ شَيْءٍ فَعَلُوهُ فِي الزُّبُرِ
( 52 ) Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُّسْتَطَرٌ
( 53 ) Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ
( 54 ) Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍ
( 55 ) Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.