Swahili
Surah Ash-Shams ( The Sun ) - Aya count 15
وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا
( 1 ) Naapa kwa jua na mwangaza wake!
وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا
( 2 ) Na kwa mwezi unapo lifuatia!
وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا
( 3 ) Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا
( 4 ) Na kwa usiku unapo lifunika!
وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا
( 5 ) Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا
( 6 ) Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا
( 7 ) Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا
( 8 ) Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا
( 9 ) Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا
( 10 ) Na hakika amekhasiri aliye iviza.
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا
( 11 ) Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا
( 12 ) Alipo simama mwovu wao mkubwa,
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ نَاقَةَ اللَّهِ وَسُقْيَاهَا
( 13 ) Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا
( 14 ) Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا
( 15 ) Wala Yeye haogopi matokeo yake.