Swahili
Surah Ad-Dukhan ( The Smoke ) - Aya count 59
حم
( 1 ) H'a Mim
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ
( 2 ) Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha,
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
( 3 ) Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ
( 4 ) Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima,
أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ
( 5 ) Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
( 6 ) Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
( 7 ) Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ
( 8 ) Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ
( 9 ) Lakini wao wanacheza katika shaka.
فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ
( 10 ) Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri,
يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ
( 11 ) Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu!
رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ
( 12 ) Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ
( 13 ) Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ
( 14 ) Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.
إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ
( 15 ) Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
( 16 ) Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ
( 17 ) Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
( 18 ) Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
( 19 ) Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ
( 20 ) Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ
( 21 ) Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.
فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ
( 22 ) Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu.
فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
( 23 ) Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ
( 24 ) Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.
كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
( 25 ) Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!
وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ
( 26 ) Na mimea na vyeo vitukufu!
وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ
( 27 ) Na neema walizo kuwa wakijistareheshea!
كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ
( 28 ) Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ
( 29 ) La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ
( 30 ) Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,
مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ
( 31 ) Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.
وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ
( 32 ) Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.
وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ
( 33 ) Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ
( 34 ) Hakika hawa wanasema:
إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ
( 35 ) Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
( 36 ) Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَاهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ
( 37 ) Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ
( 38 ) Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo.
مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
( 39 ) Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ
( 40 ) Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.
يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
( 41 ) Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
( 42 ) Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ
( 43 ) Hakika Mti wa Zaqqum,
طَعَامُ الْأَثِيمِ
( 44 ) Ni chakula cha mwenye dhambi.
كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ
( 45 ) Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
كَغَلْيِ الْحَمِيمِ
( 46 ) Kama kutokota kwa maji ya moto.
خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ
( 47 ) (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ
( 48 ) Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ
( 49 ) Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ
( 50 ) Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ
( 51 ) Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani,
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
( 52 ) Katika mabustani na chemchem,
يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ
( 53 ) Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana,
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ
( 54 ) Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini.
يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ
( 55 ) Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ
( 56 ) Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,
فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
( 57 ) Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
( 58 ) Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ
( 59 ) Ngoja tu, na wao wangoje pia.