Swahili
Surah Al-Layl ( The Night ) - Aya count 21
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ
( 1 ) Naapa kwa usiku unapo funika!
وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
( 2 ) Na mchana unapo dhihiri!
وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ
( 3 ) Na kwa Aliye umba dume na jike!
إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ
( 4 ) Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ
( 5 ) Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ
( 6 ) Na akaliwafiki lilio jema,
فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ
( 7 ) Tutamsahilishia yawe mepesi.
وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ
( 8 ) Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ
( 9 ) Na akakanusha lilio jema,
فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ
( 10 ) Tutamsahilishia yawe mazito!
وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ
( 11 ) Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ
( 12 ) Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ
( 13 ) Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ
( 14 ) Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى
( 15 ) Hatauingia ila mwovu kabisa!
الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
( 16 ) Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى
( 17 ) Na mchamngu ataepushwa nao,
الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ
( 18 ) Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ
( 19 ) Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ
( 20 ) Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ
( 21 ) Naye atakuja ridhika!