Swahili
Surah Al-Ma'arij (The Ways of Ascent ) - Aya count 44
سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ
( 1 ) Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea,
لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ
( 2 ) Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia -
مِّنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ
( 3 ) Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.
تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ
( 4 ) Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!
فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا
( 5 ) Basi subiri kwa subira njema.
إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا
( 6 ) Hakika wao wanaiona iko mbali,
وَنَرَاهُ قَرِيبًا
( 7 ) Na Sisi tunaiona iko karibu.
يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ
( 8 ) Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa.
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ
( 9 ) Na milima itakuwa kama sufi.
وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا
( 10 ) Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake.
يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ
( 11 ) Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe,
وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ
( 12 ) Na mkewe, na nduguye,
وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ
( 13 ) Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu,
وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ
( 14 ) Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ
( 15 ) La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,
نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ
( 16 ) Unao babua ngozi ya kichwa!
تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ
( 17 ) Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka.
وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ
( 18 ) Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا
( 19 ) Hakika mtu ameumbwa na papara.
إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا
( 20 ) Inapo mgusa shari hupapatika.
وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا
( 21 ) Na inapo mgusa kheri huizuilia.
إِلَّا الْمُصَلِّينَ
( 22 ) Isipo kuwa wanao sali,
الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ
( 23 ) Ambao wanadumisha Sala zao,
وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ
( 24 ) Na ambao katika mali yao iko haki maalumu
لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ
( 25 ) Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba;
وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ
( 26 ) Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,
وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ
( 27 ) Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ
( 28 ) Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo.
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ
( 29 ) Na ambao wanahifadhi tupu zao.
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
( 30 ) Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi -
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ
( 31 ) Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ
( 32 ) Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ
( 33 ) Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,
وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
( 34 ) Na ambao wanazihifadhi Sala zao.
أُولَٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ
( 35 ) Hao ndio watakao hishimiwa Peponi.
فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ
( 36 ) Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu?
عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ
( 37 ) Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!
أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ
( 38 ) Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema?
كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ
( 39 ) La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua.
فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ
( 40 ) Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
( 41 ) Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
( 42 ) Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa,
يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ
( 43 ) Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo,
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ
( 44 ) Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa.