Swahili
Surah At-Tariq ( The Night-Comer ) - Aya count 17
وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ
( 1 ) Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ
( 2 ) Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
النَّجْمُ الثَّاقِبُ
( 3 ) Ni Nyota yenye mwanga mkali.
إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ
( 4 ) Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ
( 5 ) Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ
( 6 ) Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ
( 7 ) Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ
( 8 ) Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ
( 9 ) Siku zitakapo dhihirishwa siri.
فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ
( 10 ) Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ
( 11 ) Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ
( 12 ) Na kwa ardhi inayo pasuka!
إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ
( 13 ) Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ
( 14 ) Wala si mzaha.
إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا
( 15 ) Hakika wao wanapanga mpango.
وَأَكِيدُ كَيْدًا
( 16 ) Na Mimi napanga mpango.
فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا
( 17 ) Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.