Swahili
Surah Abasa ( He frowned ) - Aya count 42
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ
( 1 ) Alikunja kipaji na akageuka,
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ
( 2 ) Kwa sababu alimjia kipofu!
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ
( 3 ) Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ
( 4 ) Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ
( 5 ) Ama ajionaye hana haja,
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ
( 6 ) Wewe ndio unamshughulikia?
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
( 7 ) Na si juu yako kama hakutakasika.
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ
( 8 ) Ama anaye kujia kwa juhudi,
وَهُوَ يَخْشَىٰ
( 9 ) Naye anaogopa,
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ
( 10 ) Ndio wewe unampuuza?
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ
( 11 ) Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ
( 12 ) Basi anaye penda akumbuke.
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ
( 13 ) Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ
( 14 ) Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ
( 15 ) Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
كِرَامٍ بَرَرَةٍ
( 16 ) Watukufu, wema.
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ
( 17 ) Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ
( 18 ) Kwa kitu gani amemuumba?
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ
( 19 ) Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ
( 20 ) Kisha akamsahilishia njia.
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ
( 21 ) Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ
( 22 ) Kisha apendapo atamfufua.
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ
( 23 ) La! Hajamaliza aliyo muamuru.
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ
( 24 ) Hebu mtu na atazame chakula chake.
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا
( 25 ) Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا
( 26 ) Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا
( 27 ) Kisha tukaotesha humo nafaka,
وَعِنَبًا وَقَضْبًا
( 28 ) Na zabibu, na mimea ya majani,
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا
( 29 ) Na mizaituni, na mitende,
وَحَدَائِقَ غُلْبًا
( 30 ) Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا
( 31 ) Na matunda, na malisho ya wanyama;
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ
( 32 ) Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ
( 33 ) Basi utakapo kuja ukelele,
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ
( 34 ) Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ
( 35 ) Na mamaye na babaye,
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ
( 36 ) Na mkewe na wanawe -
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ
( 37 ) Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ
( 38 ) Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ
( 39 ) Zitacheka, zitachangamka;
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ
( 40 ) Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ
( 41 ) Giza totoro litazifunika,
أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ
( 42 ) Hao ndio makafiri watenda maovu.